Monday, 29 July 2024

Jua Sababu Zinazopelekea Kutoka kwa Mimba

 VYANZO VIKUU VYA MIMBA KUHARIBIKA NI:



1. Chango la Uzazi.


2. P. I. D


3. Athari zinazotokana na kutumia dawa za uzazi wa mpango hapo kabla.


4. Uvimbe kwenye kizazi.


5. Historia ya kuharibikiwa kwa mimba.


6. Msongo wa mawazo, makasiriko n.k


7. Kupanda bodaboda ukiwa mjamzito au kusafiri umbali mrefu n.k


8. Kufanya kazi ngumu ngumu wakati wa ujauzito mfano kunyanyua, kubeba, kusogeza na hata kuinama mda mrefu. 


9. Kutumia dawa kihorela bila ushauri mzuri wengine hata vinywaji vyenye kemikali nyingi n.k.


Kama ulishawahi kuharibikiwa mimba, Je, wewe unadhani namba ngapi inakuhusu hapo?.

#Dr Mzamilu Baraka 0684362870

Thursday, 25 July 2024

Njia Saba za kutumia ili Mwanamke apate Mimba.

 NJIA SABA ZA KUTUMIA ILI MKE APATE MIMBA KIRAHISI. 



1.Kufanya tendo la ndoa katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai.


'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.


2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.


3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.


Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.


4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.


5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.


6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up.


How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.


7Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.


Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.


Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto...


SHARE ELIMU HII KISHA LIKE PAGE HII KAMA BADO

Wednesday, 24 July 2024

ZITAMBUE SIKU ZA KUNASA UJAUZITO

 #ZITAMBUE SIKU HATARI ZA KUPATA MIMBA




Kwa wastani,mzunguko wa hedhi ni siku 28.

Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza mwanamke anapoanza ku-bleed



Mzunguko Wa Hedhi Wa Kawaida Una Sifa Madhubuti


1.IDADI YA SIKU KATIKA MZUNGUKO MMOJA


Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (ambapo hapo ndipo unapata wastani wa siku 28 yaani [(21+35)÷2].


Kwahiyo ndugu msomaji usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke una siku 28,hiyo si sawa wengine wana siku 27,wengine 25,wengine 35,wengine 29, wengine 33 nakadhalika hutegemeana na hali ya mwili wa mwanamke 




2.SIFA YA PILI NI UWIANO WA IDADI YA SIKU ZA MZUNGUKO KATI YA MZUNGUKO MMOJA NA MWINGINE


Hii ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la ufanyaji wa tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatarishi kwa mwanamke kupata mimba.




Ili tuseme mwanamke anamizunguko ya hedhi iliyo sawa[regular cycles],idadi ya siku za mizunguko ya hedhi kati ya mwezi na mwezi isitofautiane kwa zaidi ya wiki moja yaani siku 7 


Kwa mfano,kama mwezi wa kwanza aliona siku zake baada ya siku 28,mwezi wapili akaona baada ya siku 30,mwezi wa tatu akaona baada ya siku 35 bado mzunguko wake uko kwenye uwiano mzuri[regular cycle] kwasababu mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.



Usikariri kuwa siku za mzunguko kwa kila mwanamke ni siku 28,hiyo ni kosa kubwa.Hiyo 28 ni wastani tu.



Pia tambua ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyohuyo



Kwa mfano usitarajie kuwa kama mwezi march ame bleed baada ya siku 28 na mwezi april pia ata bleed baada ya siku 28,sio lazima iwe hivyo lakini pia inaweza tokea.


Kwa mfano mwanamke mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28,mzunguko unaofuata baada ya siku 27,mzunguko mwingine baada ya siku 30,mzunguko mwingine baada ya siku 29,mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa(tofauti si zaidi ya siku 7).




3.IDADI YA SIKU ZA KUBLEED[MENSTRUAL PERIOD]


Usichanganye kati ya menstrual period na menstrual cycle,hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.



Siku ya kwanza ya kubleed ndo siku tunayoanza kuhesabu mzunguko wa hedhi[day one],sio siku ya kumaliza ku-bleed. Kwa kawaida idadi ya siku za ku-bleed ni kati ya siku 3 hadi 7,kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo.



4. SIFA YA MWISHO YA MZUNGUKO WA HEDHI NI WINGI WA DAMU


Damu inayotoka wakati wa hedhi mwanamke anaweza ku-bleed kawaida[normal bleeding] au ku-bleed sana[heavy bleeding].


#ILI KUZIFAHAMU VIZURI SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA MIMBA HEBU TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARY.



Mzunguko wa ovary[ovarian cycle) ndio unaoleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi(menstrual cycle).


Mzunguko wa ovary una hatua zifuatazo

Follicular phase,ovulation na luteal phase.


1.FOLLICULAR PHASE


Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke ku bleed mpaka yai linapokuwa limekomaa


Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa wakati akiwa tumboni mwa mama.


Mpaka kufikia kuvunja ungo,mwanamke anakuwa na mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovary,mayai haya huwa katika hatua ya uchanga[primary oocyte].


2.OVULATION


Katika hatua hii ya mzunguko wa ovary,yai lililokomaa[graafian follicle] hutoka kwenye ovary na kuingia kwenye mirija ya fallopian.



#SASA TUTAITAMBUAJE SIKU YA YAI KUTOKA ( OVULATION )???


Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.Fuatilia hapo chini.


3.LUTEAL PHASE: hii ni sehemu ya mzunguko wa ovary ambayo huanza baada ya yai kutoka[ovulation] na kuishia kabla ya kuanza ku bleed[mwanzo wa mzunguko mwingine).


#ZINGATIA_HAPA


Idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa[mfano,28,30,35,25).


Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.


#ANGALIA HESABU HII RAHISI


Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14,kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.



Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14(luteal phase)=16,kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30,ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14(kuwa makini hapo).



Yule mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation day ni 35-14 = 21,kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.



Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia.



#KWANINI?


Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24 tangu lilipotoka kwenye ovary.



Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.



Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.

Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation



Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.



#SASA BASI KWA KUWA NIMESEMA HATUWEZI KUWA NA UHAKIKA WA 100% WA SIKU YA OVULATION NDO MAANA HUWA TUNATUMIA KANUNI YA KUEPUKA NGONO KWA KIPINDI CHA WIKI NZIMA[7 DAYS] AMBAZO NI SIKU ZILIZO KARIBU SANA NA SIKU YA OVULATION KWA WALE WANAOTUMIA CALENDER METHOD.


Mfano,kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16,kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza.sasa kama ni siku ya 16,ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo,acha ngono.




Pia jumlisha siku 3 mbele,ambapo mwanamke atatakiwa kuanza ngono kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba 



#USHAURI:


Ila kwa wana ndoa ambao wanahitaji mtoto hizo siku za hatari ndio mcheze nazo, kama wote mpo vizuri yaani hamna shida kwenye uzazi basi kwa uwezo wa ALLAH basi mwanamke atashika ujauzito. Endelea kujaribu kila mwezi siku hizo za hatari. Pia wanandoa hawa wanatakiwa kufanya tendo hili zaidi ya mara moja moja hasa wakati wa tarehe za hatari


Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa:


Simu/whatsapp: 0684362870

Thursday, 11 July 2024

Jinsi ya kuweza kuosha Uke.

 Jinsi gani unaweza kuosha uke?

Kuhakikisha uke ni safi na wenye afya ni muhimu kwa afya ya uzazi na kuepuka maambukizi. Hapa kuna njia salama na sahihi za kuosha uke:


Tumia Maji Safi na Vuguvugu: Tumia maji safi na ya vuguvugu kuosha sehemu za nje za uke. Epuka kutumia maji ya moto ambayo yanaweza kusababisha kuwasha au kukausha ngozi.


Epuka Sabuni Kali: Usitumie sabuni zenye harufu kali au kemikali nyingi kwani zinaweza kuvuruga uwiano wa pH na kusababisha maambukizi. Ikiwa ni lazima kutumia sabuni, chagua sabuni laini isiyo na harufu maalum kwa ajili ya sehemu za siri.


Epuka Douche: Douche (kuosha uke kwa kutumia dawa maalum au maji yenye kemikali) inaweza kuondoa bakteria wazuri na kuvuruga uwiano wa bakteria kwenye uke, na hivyo kuongeza hatari ya maambukizi.


Osha Sehemu za Nje Tu: Uke una mfumo wake wa kujisafisha, hivyo ni muhimu kuosha sehemu za nje pekee (vulva). Epuka kuingiza kitu chochote ndani ya uke wakati wa kuosha.


Kukauka Vizuri: Baada ya kuosha, hakikisha unakauka vizuri kwa kutumia taulo safi. Epuka kutumia taulo yenye unyevu ambayo inaweza kuwa na bakteria.


Vaa Nguo za Pamba: Pamba inaruhusu hewa kupita na kusaidia uke kubaki mkavu. Epuka nguo za ndani za nailoni au nyingine zisizopitisha hewa.


Badilisha Nguo za Ndani Mara kwa Mara: Badilisha nguo za ndani kila siku na wakati unapokuwa na hedhi, hakikisha unabadilisha pedi au tampon mara kwa mara.


Kuwa Makini na Vitu vya Kujisafisha: Hakikisha vitambaa, taulo, na nguo za ndani unazotumia ni safi na zimekaushwa vizuri.


Jiepushe na Kemikali na Harufu: Epuka kutumia manukato, poda, au bidhaa nyingine zenye harufu katika eneo la uke.


Kwa kufuata hatua hizi, unaweza kusaidia kuhakikisha uke wako unabaki safi na wenye afya. Ikiwa una dalili zozote za maambukizi kama vile harufu isiyo ya kawaida, kuwasha, au kutokwa na uchafu wa rangi isiyo ya kawaida, ni muhimu kutembelea daktari kwa uchunguzi na matibabu sahihi.

Kama unachangamoto yoyote ya Uzazi wasiliana nasi kwa namba 0684362870

Monday, 8 July 2024

Yafaham mambo yanayoweza kukusaidia unase ujauzito Haraka

 



Haya ni maswali yanayohusiana na uzazi na afya ya uzazi. Ingawa ni muhimu kutafuta ushauri wa kitaalamu kwa masuala haya, hapa kuna baadhi ya maelezo ya jumla:


Vidonge vya kushika mimba HARAKA:

 Vidonge vya uzazi wa mpango (fertility pills) vinaweza kusaidia baadhi ya wanawake kupata mimba haraka. Vidonge hivi husaidia kusawazisha homoni na kuboresha uwezo wa uzazi. Ni muhimu kuwasiliana na daktari kwa ushauri wa matumizi.


Dawa ya kupata ute wa mimba:

Ute wa uzazi (cervical mucus) ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha safari ya mbegu za kiume kufikia yai. Kuna dawa na virutubisho vinavyoweza kusaidia kuboresha ute wa uzazi, kama vile vitamini E, omega-3, na dawa za homoni.


Dawa ya miti shamba ya kupata mimba:

 Baadhi ya mimea ya asili imekuwa ikitumika kwa karne nyingi kuboresha uzazi. Mimea kama vile maca, vitex (chasteberry), na shatavari zinajulikana kwa kusaidia afya ya uzazi. Ni muhimu kutumia dawa hizi chini ya usimamizi wa mtaalamu wa dawa za asili.


Dawa ya asili ya kushika mimba HARAKA:

 Mbali na miti shamba, kuboresha lishe, kudhibiti msongo wa mawazo, na kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kusaidia. Vyakula vyenye folic acid, zinc, na vitamini B6 vinaweza kuwa na manufaa kwa uzazi.


Dawa ya kupata mimba kwa HARAKA pdf:

 Tafuta nyaraka au vitabu vya kitaalamu vinavyotoa mwongozo juu ya mbinu za kuboresha uzazi. Vitabu hivi mara nyingi vinaeleza kuhusu mlo bora, mazoezi, na njia za kiafya za kuongeza nafasi ya kupata mimba.


Jinsi ya kupata mimba baada ya hedhi: Kupata mimba baada ya hedhi inategemea muda wa mzunguko wa hedhi yako. Siku za kupevusha (ovulation) kawaida ni kati ya siku ya 11 hadi 21 kutoka siku ya kwanza ya hedhi. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara wakati huu kunaweza kuongeza nafasi ya kupata mimba.


Ni muhimu sana kuwasiliana na daktari au mtaalamu wa afya ya uzazi kwa ushauri wa kina na sahihi kulingana na hali yako binafsi.

Au Unaweza kuwasiliana nasi kwa namba +255684362870