Friday, 30 August 2024

Athari za KUJICHUA Ukeni

 Kujichua (au kujipiga punyeto) ni tendo la kujipa raha kwa kutumia mikono au njia nyingine bila kushirikisha mtu mwingine. Ingawa kujichua kwa kiasi kidogo hakusababishi matatizo makubwa kiafya, kuna athari zinazoweza kutokea, hasa ikiwa tendo hili linafanyika kwa kupindukia. Baadhi ya athari zinazoweza kutokea ni:



Kulevya na Kusababisha Utegemezi: Kujichua mara kwa mara kunaweza kusababisha utegemezi ambapo mtu anakuwa hawezi kujizuia na anahitaji kufanya tendo hili mara kwa mara ili kupata raha.


Kuharibu Mahusiano: Watu wanaojichua sana wanaweza kukosa hamu ya kushiriki ngono na wenzi wao, jambo ambalo linaweza kuharibu uhusiano wao wa kimapenzi.


Msongo wa Mawazo na Hatia: Watu wengine wanaweza kupata msongo wa mawazo, huzuni, au hisia za hatia baada ya kujichua, hasa ikiwa wanaamini kwamba ni tendo lisilofaa kimaadili au kidini.


Kupunguza Nguvu za Kiume: Ingawa si jambo la kawaida, baadhi ya wataalam wanaamini kwamba kujichua sana kunaweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume na hata kushindwa kupata au kudumisha uume uliosimama.


Kupunguza Hamu ya Kufanya Kazi au Kazi za Kawaida: Kujichua kwa kupindukia kunaweza kusababisha mtu kukosa hamu ya kufanya kazi au kushiriki katika shughuli za kawaida, kwani nguvu na mawazo yake yote yanaweza kuelekezwa kwenye tendo hilo.


Madhara ya Kimwili: Kujichua kupita kiasi kunaweza kusababisha kuumia kwenye sehemu za siri, kama vile kuchubuka ngozi au kuvimba kwa uume au uke.


Ni muhimu kuzingatia kwamba kujichua kwa kiwango cha wastani na kwa mtazamo wa afya hakusababishi matatizo makubwa, lakini kama mtu anahisi kwamba anafanya kwa kupindukia au anakumbwa na athari yoyote hasi, ni vyema kutafuta msaada kutoka kwa mtaalamu wa afya ya akili au daktari.


Tupigie kwa Ushauri na Matibabu kwa namba zetu za Ofisi +255684362870

MADHARA YA KUJICHUA (PUNYETO) KWA WANAWAKE

 *MADHARA YA KUJICHUA(PUNYETO) KWA WANAWAKE*



Wanawake wengi leo hii wamekuwa wahanga wa tatizo hili la kujichua kwa kile wanachodai kuto rizishwa na wenza wao badala yake hutumia vidole au vitu mbalimbali kujichua na kujiridhisha wenyewe.Kitendo hiki wengi hukifanya wakiwa wanaimani hakina madhara au watafanya kwa mda tu wataacha,lakini uhalisia ni kwamba yapo madhara mengi ya jambo hili,leo tuangalie haya machache..


1.KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA;

Kujichua ni kitendo kinacho husisha ubongo na homon katika mwili,unapofanya kitendo hiki sehem zako za siri zitapata sugu ambayo itapelekea ukose ham na radha hata pindi unapokutana na mwenza wako.


2.MARADHI;

 Magonjwa kama UTI sugu na Fangasi yamekuwa sugu yani hayaponi kwa watu wanaojichua na hii inatokana na usafi wa vitu vunavyotumika kujichua na ulaini wa sehem zako a siri.


3.KANSA KATIKA SHINGO YA KIZAZI; 

kuna baadhi ya wanawake hutumia ndizi,vifaa vya plastiki au chochote kuingia sehem za siri wakati wa kufanya tendo hili,hii ni hatari kubwa kwa maana inaweza kukupelekea kupata kansa katika via vyak vya uzazi.


4.KUSHINDWA KUPATA MIMBA; 

Kama utakuwa umefanya kitendo hiki kw mrefu,kumbuka sehem zako za siri zitakuwa na sugu na pia zitakosea ul ute wa uzazi unaotumika kusafirisha mbegu za kiume hadi kwenye mji wa mimba,ukifikia kiwango hiki sahau kupata mtoto.


✍MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA;

 Hii inatokana na kufa kwa tezi zinazohusika kuzalisha ute pale ukeni,kufa kwa tezi hizi kutafanya sehem yako ya siri iwe kavu,ukavu huu ndio unaopelekea maumivu makali pindi unapofanya tendo la ndoa kutokana na mchubuko mkali unaotengenezwa kwa kukosa ute wakutosha.


5.MAAMBIKIZI YA HIV/AIDS; 

Mtu alie athirika na punyeto ni rahisi sana kupata maambukizi ya ukimwi pindi akikutana na muathirika hii ni kwasababu uke wake unakuwa hauna ute hivyo msuguano ni mkubwa wakati wa tendo la ndoa,hii itamfanya apate virusi mapema.


*JE KUNA DAWA YA KUACHA KUJICHUA*

✍Wanawake wengi mara baada ya kuona wameathirika na jambo hilo huwa wanatamani kuacha lakini kila wakijaribu huwa wanashindwa,yani anaacha siku chache halafu anarudia tena,hii ni hatari sana kwako..kama wewe ni miongoni mwao yani umeshindwa kabisa kuacha tabia hii, usijari zipo njia za kufuata kuacha kitendo hiki, Tuna mfumo wa Tiba lishe na Ushauri wa Kiafya ili Kutibu Tatizo hili moja kwa moja.


Tupigie/Call/Whatsap

📞📲  +255684362870

Thursday, 29 August 2024

JE, HEDHI YAKO NI SALAMA?

 *Je, Hedhi Yako Ni SALAMA* ?



Hedhi ni kipindi maalumu katika mzunguko wa siku za mwanamke mwenye umri wa kushika Mimba


Hedhi bora ni ishara ya afya njema ya uzazi.


Kama unaona kitu hakipo sawa katika hedhi yako, ni muhimu kupata ushauri na msaada wa wataalamu wa afya. 


 *Hedhi bora ina sifa hizi* :


*Hedhi Mara Moja kwa Mwezi* : Ikiwa mzunguko wako ni siku 28, hedhi inatakiwa kupatikana kila baada ya siku 28. Hedhi isiyokuwa na mzunguko thabiti inaweza kuwa ishara ya shida.


*Hedhi Kila Mwezi* : Mwanamke anatakiwa kupata hedhi kila mwezi. Ikiwa miezi inapita bila hedhi, hiyo ni ishara ya tatizo linalohitaji tiba.


*Kiasi cha Damu* : Hedhi bora si nzito sana wala nyepesi sana. Haipaswi kuwa na vinyama nyama au vipande vya maini.


*Maumivu* : Maumivu makali yanapaswa kutokuwa sehemu ya hedhi yako. Hedhi yenye maumivu makali inahitaji uchunguzi na ushauri wa kitaalamu.


*Mabadiliko ya Mwili* : Hedhi isiyo bora inaweza kusababisha mabadiliko kama kuvimba usoni au kuwa na chunusi nyingi.


*Muda wa Hedhi* : Hedhi inapaswa kudumu siku 3 mpaka 7. Muda chini ya hapo au zaidi ni ishara ya tatizo.


*Harufu* : Hedhi bora haina harufu mbaya. Harufu mbaya inaweza kuwa dalili ya maambukizi ya bakteria na inahitaji matibabu.


 *Je, unahisi hedhi yako ipo salama?* 


Ikiwa kuna changamoto yoyote ya hedhi unayopitia, ni wakati wa kutafuta msaada.


 Wasiliana nasi ili kupata ushauri na tiba sahihi kwa afya bora ya uzazi.


Tupigie kwa namba +255684362870

Saturday, 24 August 2024

KWANINI DAWA NYINGI UNAZOTUMIA HAZIKUSAIDII KUNASA UJAUZITO?

 *Kwanini Dawa Nyingi Unazotumia Hazikusaidii Kupata Ujauzito?*



Wanawake wengi sana wanafanya kosa hili hapa pindi wanapotaka kubeba mimba. Kosa lenyewe ni kuwa,


Wanapomwona mwanamke mwenzao ambaye alihangaika kupata ujauzito na baadae wanamwona amepata ujauzito. 


Wanaanza kwa kuuliza ni dawa gani iliyomsidia mwanamke huyo kupata ujauzito? 


Matokeo yake ni kwamba, jibu watakalopata ndio wanaanza sasa kuitafuta dawa hiyo ili na wao waitumie.


Wanafanya hivyo bila kujua, mwenzao alikuwa anasumbulia na nini na ile dawa ilienda kutibu nini hadi mwenzao kapata ujauzito. 


Mwisho wa siku wanajikuta kuwa wameshaipata hiyo dawa na wanaanza kutumia.


Watatumia hadi itakapoisha, na baadae wanashangaa siku, wiki, miezi, miaka inapita.


Wao hawapati ujauzito, wakati mwenzao alitumia dawa hiyo hiyo kabla hata hajamaliza dozi alipata ujauzito. 


Happ ndipo unaanza kujiuliza tatizo liko wapi, mbona haujapata ujauzito kama mwenzako?


Jambo usilolijua ni kuwa, dawa haina shida nasema hivi kwasababu kila dawa unayoiona.


Imetengezwa kwa ajili ya kutatua tatizo fulani. Kwahiyo ikiwa dawa hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya kumaliza hilo tatizo.


Basi muhusika (au mtumiaji) wa hiyo dawa akitumia itamsaidia kumaliza tatizo alilokuwa nalo na atapata mtoto.


Wakati huo huo kwa mwingine akitumia dawa hiyo hiyo, haiwezi kumsaidia na kupata mtoto.


Kwasababu tatizo ulilo nalo wewe sio sawa na tatizo alilo nalo mwenzako.


Kwahiyo, kabla ya kutumia dawa yoyote ile hakikisha ya kwamba unajua tatizo ulilo kuwa nalo na unajua kuwa hiyo dawa inaenda kutatua tatizo hilo ulilo nalo 


Vinginevyo zaidi ya hapo, utatumia dawa ya kila aina, dawa za kila kampuni, utatumia dawa za hospitali na za kienyeji.


Utapoteza pesa nyingi, lakin ikiwa dawa utakayotumia haiendani na tatizo ulilo kuwa nalo huwezi kupata ujauzito. 


Utabaki kushuhudia tu kwa wenzako, halafu kwako unashangaa kwanini dawa inadunda?


Jibu ni rahisi tu, TATIZO lako na kazi inayoenda kufanya DAWA utakayotumia ni vitu viwili tofauti. Ndio maana tatizo lako haliishi.


Suluhisho lake ni nini sasa? 


Suluhisho pekee ni wewe kujua chanzo cha tatizo lako (au kutobeba mimba) ni nini?


Ukishajua tafuta mtaalamu atakaekusaidia kukupatia tiba itakayoenda kumaliza hilo tatizo lako.


Ukifanya hivi utapata ujauzito. Vinginevyo ni shuhuri pevu.


Labda nikuuibie tu siri. 


Matatizo mengi ambayo yanawakumba wanawake na yanayosababisha wasibebe mimba, tatizo kubwa ni moja tu, ambalo ni...


... HORMONAL IMBALANCE (kuvurugika kwa homoni)


Hayo matatizo mengine unayoyaona wewe, matatizo kama vile...


Uvimbe kwenye kizazi au mfuko wa mayai, kutoona siku zako, hedhi isiyo na mpangilio, kutokwa na mabonge (au kama vipande vya nyama) wakati wa hedhi.


Kupata maumivu makali wakati unakaribia hedhi au wakati wa hedhi yenyewe, matiti kuuma (au kujaa), kukosa ute wa uzazi,


Kukosa hamu ya tendo la ndoa, kutofurahia tendo, ukavu ukeni, kutokwa na hedhi nyeusi sana, n.k


Matatizo yote hayo huwa yanasababishwa na HOMON IMBALANCE. 


Tatizo ni kwamba wengi wanapotaka kutatua changamoto hizo.


Huwa wanadili na tatizo kama lilivyo na sio kiini cha tatizo ambacho ni kuvurugika kwa homoni.


Kwa mfano, mtu ana uvimbe kwenye kizazi baada ya kutibu kiini cha tatizo huwa anataka kuondoa tatizo lilioko ambalo ni kuondoa UVIMBE.


Uvimbe huu atauondoa kwa njia mbalimbali mfano kufanyiwa upasuaji au kuchukua dawa itakayoondoa uvimbe huo.


Na huku anasahau kuweka homoni zake sawa.


Na hapo ndipo anapokuja kushangaa, uvimbe umeisha lakini mimba habebi. Kwanini?...


Kwasababu, kiini cha tatizo hakijaondolewa ambacho ni homoni kutokuwa sawa.


Na hata kwenye upande wa homoni, hii ni mada pana sana. Kwani...


Kuvurugika kwa homoni maana yake ni kwamba aidha homoni zinazidi kuliko kawaida au zinapungua kuliko kawaida.


Huenda ikawa wanawake wawili wote wana tatizo la homoni kutokuwa sawa.


Lakini, matibabu yake huwa tofauti na mwingine. Kwasababu ya dalili watakazoonyesha watu hawa.


Kiufupi ni kwamba, dawa zote unazotumia kuweka homoni sawa ni za muda mfupi.


Yaani zinafanya kazi ndani ya muda mfupi tu. Baada ya muda huo kupita hali inarudi pale pale.


Hii yote ni kwasababu ya mtindo wa maisha tunayoishi, madawa tunayotumia, vyakula tunavyokula (vingi vina kemikali na vimetoka viwandani)


Mafuta tunayotumia (ya kupaka au ya kupikia), vipodozi unavyotumia, n.k.


Kwahiyo, njia pekee itakayoweza kukusaidia ni wewe kutumia dawa hizo ambazo zitakusaidia kuweka homoni zako sawa.


Lakini pia, upate muongozo mzuri utakokusaidia ku mantain hizo homoni zako zisivurugike tena.


Nina mengi ya kukuambia, lakini acha tu tuishie hapa. 


Haya yote niliyokuambia ni matokeo niliyoyapata baada ya kuongea na baadhi ya wanawake wenye Changamoto za KUTOSHIKA MIMBA ndo nimekuja kugundua hayo. 


Kwahiyo wewe kuwa makini hata pale utakapo nunua dawa basi jitahidi ufahamu na namna itakayokuwezesha ku maintain homoni zako  zisicheze tena baada ya kumaliza kutumia dawa.


Nakutakia mafanikio mema!


Mimi ndugu yako.


Mzamilu Baraka

Thursday, 22 August 2024

Kwanini Wanandoa wengi Hawaponi Fangasi Sehem Za Siri?

 Sababu kuu wanandoa wengi wanashindwa kupona fangasi sehemu za siri ni:



Matibabu yasiyokamilika: Watu wengi wanaweza kuacha matibabu mara tu dalili zinapoanza kupungua, badala ya kumaliza dozi kamili iliyopendekezwa na daktari, na hivyo fangasi wanaweza kurudi.


Madhara ya dawa za kujitibu: Watu wengine wanatumia dawa bila ushauri wa daktari au kutumia tiba za kienyeji ambazo zinaweza kuwa hazifai au hata kuzidisha tatizo.


Mabadiliko ya tabia: Wanandoa wengi wanahitaji kubadilisha baadhi ya tabia kama vile usafi wa mwili, kubadili mara kwa mara nguo za ndani, na kuepuka nguo za kubana. Bila mabadiliko haya, fangasi wanaweza kuendelea kujirudia.


Maambukizi ya pande zote: Ikiwa mwenzi mmoja anapata matibabu na mwingine hapati, kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi kuendelea kurudi. Ni muhimu wanandoa wote wawili kupata matibabu wakati huo huo.


Kushindwa kudhibiti vyanzo vya mazingira: Mazingira yenye unyevunyevu, matumizi ya sabuni zenye kemikali kali, au vyoo visivyo safi vinaweza kuchangia kuendelea kwa fangasi.


Magonjwa mengine yanayoathiri kinga: Watu wenye magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili kama vile kisukari au VVU wanaweza kuwa na ugumu zaidi kupona kabisa kutokana na fangasi.


Kufanikiwa kupona fangasi kunahitaji matibabu sahihi, mabadiliko ya tabia, na ushirikiano wa wanandoa wote wawili.


Je, umesumbuliwa na Changamoto hii ya Fangasi kwa kipindi kirefu bila mafanikio?


Tupigie kwa Ushauri na Matibabu kwa namba zetu +255684362870

ZIJUE NJIA RAHISI ZA KUONDOKANA NA FANGASI UKENI

 Kutibu fangasi ukeni, unaweza kutumia njia kadhaa:



1. Dawa za Kiasili


Mafuta ya mti wa chai (Tea Tree Oil): Yanajulikana kuwa na sifa za kuua fangasi. Unaweza kutumia matone machache katika mafuta ya mzeituni kisha kupaka nje ya uke.


Mafuta ya Nazi: Yanasaidia kupunguza fangasi kutokana na sifa zake za kuua fangasi. Paka nje ya uke mara kwa mara.


Yogurt ya Kawaida (Plain Yogurt): Ina probiotic ambazo husaidia kudhibiti ukuaji wa fangasi. Unaweza kutumia yogurt kwa kupaka nje ya uke au kula kwa wingi.


2. Dawa za Duka la Dawa (Pharmacy)


Antifungal Creams: Kama vile clotrimazole au miconazole. Hizi ni cream ambazo hupakwa ndani na nje ya uke kwa muda wa siku kadhaa kama ilivyoelekezwa.


Suppositories: Hizi ni vidonge vinavyowekwa ndani ya uke, ambavyo husaidia kuua fangasi.


Vidonge vya Kumeza (Oral Tablets): Kama vile fluconazole, ambavyo hutumiwa kwa matibabu ya fangasi sugu. Hii ni mara moja kwa kawaida, ila daktari anaweza kuagiza mara kadhaa kulingana na hali yako.


3. Ushauri wa Lishe na Mazingira


Kula Chakula Chenye Probiotics: Chakula kama yogurt na kefir kina bakteria wazuri ambao husaidia kudhibiti fangasi mwilini.


Epuka Sukari na Vyakula vya Wanga Wingi: Sukari inajulikana kuchochea ukuaji wa fangasi, hivyo ni bora kupunguza ulaji wake.


Usafi wa Kibinafsi: Osha sehemu za siri kwa sabuni isiyo na kemikali kali na maji safi mara kwa mara.


4. Wakati wa Kumwona Daktari


Kama unapata maumivu makali, harufu mbaya, au hali inarudiarudia licha ya kutumia tiba, ni muhimu kumuona daktari ili kupata matibabu maalum.


Ni muhimu kufuata maelekezo ya daktari ikiwa dalili hazipungui au kama fangasi ni sugu.


Tupigie kwa Ushauri na Matibabu kwa namba zetu 0684362870

Wednesday, 21 August 2024

FAHAMU KUHUSU UVIMBE MAJI KWENYE MAYAI

 *Tatizo la Vijivimbe Maji kwenye Mayai*



PCOS ni ugonjwa wa mfumo wa homoni ambao huongeza kiwango cha homoni za kiume za androjeni kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. 


Homoni hii tayari ipo katika miili ya wanawake lakini kwa kiwango kidogo zaidi.


Tatizo hili husababisha kutokea au kuwa na vijivimbe maji kwenye mayai


Polycystic Ovary Syndrome (PCOS) ni hali tata ambayo huathiri wanawake katika makundi mbalimbali ya umri, na huleta changamoto tofauti katika kila hatua ya maisha. 


Hapa kuna muhtasari wa jinsi inavyoathiri wanawake, sababu zake zinazowezekana, na mikakati ya kudhibiti hali hii:


Athari za PCOS Katika Makundi Tofauti ya Umri


1. *Wasichana Balehe*:


   - *Dalili*: Mizunguko isiyo ya kawaida ya hedhi, ongezeko la uzito, na nywele nyingi mwilini (hirsutism) zinazoonekana kwa muundo wa kiume.


   - *Changamoto*: Dalili hizi zinaweza kuwa na athari ya kihisia na kisaikolojia kwa vijana hao.


2. *Wanawake wa Umri wa Kuzaa*:


   - *Hatari*: Uwezekano mkubwa wa kuharibika kwa mimba, utasa, shinikizo la damu, na kisukari wakati wa ujauzito, na kifo cha mtoto baada ya kuzaliwa.


   - *Changamoto*: Hali hii inaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa wanawake wanaotaka kupata watoto na inaweza kuhitaji matibabu maalum ya uzazi.


3. *Wanawake wa Umri Mkubwa*:


   - *Hatari*: Magonjwa sugu kama kisukari cha aina ya pili, ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, hedhi nzito, na saratani ya uterasi.


   - *Changamoto*: Hatua za kudhibiti hali hii zinahitajika ili kuzuia matatizo haya ya kiafya kwa muda mrefu.



Sababu halisi ya PCOS bado haijulikani, lakini kuna uhusiano na upinzani wa insulini, 


...ambapo mwili hutengeneza insulini zaidi kupambana na upinzani wa insulini. 


Hizi ni baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia kuendeleza PCOS:


1. *Homoni za Kiume (Androjeni)*: Uzalishaji wa androjeni, au homoni za kiume, unachangia kwa kiasi kikubwa katika PCOS kwani 


...husababisha dalili kama vile ongezeko la nywele usoni, chunusi, na mizunguko isiyo ya kawaida ya hedhi. 


Homoni hizi huzuia kuachiliwa kwa mayai.


2. *Unene*: Ingawa bado haijafahamika kama unene ni sababu au athari ya PCOS.


Kuna uhusiano kati ya vyote viwili, na kufuata mpango wa usimamizi wa uzito bora unaonekana kuwa muhimu.


3. *Urithi*: PCOS inaweza kuathiriwa na jeni maalum katika familia. 


Kuwa na historia ya familia ya PCOS inaweza pia kuchangia hali hii.


4. *Upinzani wa Insulini*: Homoni iitwayo insulini hutengenezwa na kongosho na husaidia seli kutumia sukari kama chanzo cha nishati kuu mwilini. 


Viwango vya sukari kwenye damu vinaweza kuongezeka ikiwa seli zitakuwa sugu kwa insulini. 


Mwili unaweza kujaribu kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu kwa kuzalisha insulini zaidi. 


Katika hali ya kuwa na insulini nyingi, mwili unaweza kuzalisha homoni za kiume (androjeni) nyingi zaidi, ambazo zinaweza kuingilia kati mzunguko wa hedhi. 


Hii inaweza pia kusababisha hamu kubwa ya chakula na kuongezeka kwa uzito. 


Aidha, matuta meusi, yenye velvety kwenye shingo, chini ya matiti, na kwapani yanaweza kuonekana, ambayo ni dalili za upinzani wa insulini


PCOS inaweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:


- *Lishe Bora*: Kufuata mpango wa lishe unaozingatia afya ya mwili mzima na kupunguza uzito kupita kiasi.

- *Mazoezi*: Mazoezi ya kawaida yanasaidia kuboresha matumizi ya insulini na kudhibiti uzito.

- *Dawa*: Kuna dawa maalum zinazoweza kusaidia kudhibiti dalili za PCOS, kama vile dawa za kurekebisha homoni na za kudhibiti insulini.


Kudhibiti PCOS kwa wakati unaofaa ni muhimu ili kupunguza athari zake za muda mrefu na kuboresha ubora wa maisha kwa wanawake walioathirika.


*Dalili za PCOS*


Wanawake wenye PCOS huonyesha dalili mbalimbali kulingana na hali ya afya yao. 


Hata hivyo, dalili zifuatazo ni baadhi ya zile za kawaida ambazo ni muhimu kuzitambua:


- Kukosa hedhi, mizunguko isiyo ya kawaida au mizunguko hafifu.

- Kuwa na nywele nyingi mwilini, hasa kifuani, tumboni, mgongoni, kidevuni, au usoni.

- Kuongezeka kwa uzito hasa kwenye eneo la tumbo.

- Chunusi zinazorudiarudia mara kwa mara.

- Kushindwa kushika mimba kwa njia ya kawaida.

- Kuwa na vipande vya ngozi vya ziada kwenye kwapa au shingoni.

- Kuwa na ngozi nyeusi, hasa kwenye kinena, shingo, au chini ya matiti.

- Kupoteza nywele kwa kasi au kunyonyoka kwa nywele.

Wasiliana nasi kwa namba zetu 0684362870

Sunday, 18 August 2024

MADHARA YA KUCHELEWA KUPATA UJAUZITO NI YAPI?

 Kuchelewa kupata ujauzito kunaweza kusababisha madhara kadhaa ya kiafya na ya kisaikolojia. Hata hivyo, madhara hayo hutegemea sababu na hali maalum ya mtu binafsi. Baadhi ya madhara ya kuchelewa kupata ujauzito ni:



Shinikizo la kisaikolojia: Wanawake wanaoweza kukabiliana na matatizo ya kupata ujauzito wanaweza kuhisi msongo wa mawazo, hofu, huzuni, na kupoteza matumaini.


Matatizo ya kiafya: Kuchelewa kupata ujauzito kunaweza kuashiria matatizo ya uzazi kama vile matatizo ya homoni, matatizo ya mirija ya uzazi, au magonjwa ya uzazi kama endometriosis au uvimbe kwenye mfuko wa uzazi.


Kuzorota kwa ubora wa mayai: Umri mkubwa unaweza kusababisha kupungua kwa ubora wa mayai, jambo linalopunguza nafasi ya kupata ujauzito.


Hatari ya kuharibika kwa mimba: Wanawake wanaopata ujauzito katika umri mkubwa wanakabiliwa na hatari ya juu ya kuharibika kwa mimba au matatizo mengine ya ujauzito kama vile shinikizo la damu na kisukari cha mimba.


Mahusiano: Kuchelewa kupata ujauzito kunaweza kuleta changamoto kwa mahusiano ya wanandoa kutokana na msongo wa mawazo, hisia za lawama, au upungufu wa ushirikiano wa kihisia.


Ni muhimu kutafuta ushauri wa daktari ili kufanyiwa vipimo na kupata msaada unaofaa ikiwa kuna tatizo la kuchelewa kupata ujauzito.


Kama umehangaika kwa muda mrefu kutafuta ujauzito bila mafanikio tupigie kwa namba +255684362870

ZIFAHAM HASARA ZA KUTOSHIRIKI TENDO LA NDOA KWA USAHIHI

 Kutoshiriki tendo la ndoa kiukamilifu kunaweza kuleta athari mbalimbali, ambazo zinaweza kuathiri mtu binafsi kihisia, kimwili, na kijamii. Hapa ni baadhi ya hasara za kutoshiriki tendo la ndoa kiukamilifu:



Msongo wa Mawazo na Huzuni: Kutokufanya tendo la ndoa, au kutokuridhika wakati wa tendo la ndoa, kunaweza kusababisha msongo wa mawazo, huzuni, na hisia za upweke. Watu wengi wanahusisha tendo la ndoa na uhusiano wa karibu, hivyo kutokuwepo kwa tendo hilo kunaweza kusababisha matatizo ya kihisia.


Kupungua kwa Ukaribu na Mpenzi: Katika uhusiano wa muda mrefu kama ndoa, tendo la ndoa linaweza kusaidia kudumisha ukaribu wa kihisia. Kutokuwa na tendo hilo kunaweza kusababisha wenzi kujisikia mbali au kutokuwa na urafiki wa karibu, jambo ambalo linaweza kuathiri ubora wa uhusiano.


Kupungua kwa Ujasiri: Tendo la ndoa linaweza kusaidia kuongeza ujasiri wa mtu binafsi. Kutopata uzoefu huo au kutopata kuridhika kunaweza kuathiri jinsi mtu anavyojisikia kuhusu mwili wake au jinsi anavyothaminiwa na mpenzi wake.


Shida za Kiafya: Ingawa kutoshiriki tendo la ndoa hakuathiri moja kwa moja afya ya mwili kwa kila mtu, watu wengine wanaweza kupata shida kama vile maumivu ya kichwa, kukosa usingizi, au kukosa msisimko wa jumla wa mwili. Tendo la ndoa linaweza kusaidia katika kupunguza stress, kuboresha mzunguko wa damu, na kuimarisha mfumo wa kinga.


Matatizo ya Homoni: Kwa baadhi ya watu, tendo la ndoa husaidia kusawazisha homoni, kama vile oksitosini (homoni ya furaha) na endorphins, ambazo zinasaidia katika kudhibiti stress na kutoa hisia za furaha. Kutokufanya tendo la ndoa kunaweza kusababisha upungufu wa homoni hizi, jambo ambalo linaweza kuathiri hali ya kihisia na kimwili.


Kupungua kwa Uridhiko wa Maisha: Kwa baadhi ya watu, tendo la ndoa ni sehemu muhimu ya furaha ya jumla maishani. Kutokuwepo kwa tendo hili kunaweza kusababisha hisia za kutoridhika, kutokutosheka, au hisia za kuacha jambo muhimu maishani.


Ikiwa hali hii inasababisha shida katika uhusiano au afya ya kihisia, ni vyema kutafuta msaada wa kitaalamu kwa ajili ya ushauri na mwongozo.


Kama umehangaika kupata Furaha katika TENDO LA NDOA kwa muda mrefu tupigie kwa namba zetu +255684362870.

HIZI HAPA FAIDA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

 Faida za kufanya mapenzi zipo kadhaa, na nyingi zinahusisha afya ya mwili, akili, na hali ya kijamii. Baadhi ya faida hizo ni:



Kuboresha afya ya moyo: Kufanya mapenzi mara kwa mara kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo kwa sababu huongeza mzunguko wa damu na kuboresha afya ya mishipa.


Kupunguza msongo wa mawazo: Homoni kama oxytocin na endorphin zinazotolewa wakati wa kufanya mapenzi husaidia kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo.


Kuimarisha kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara kwa mara kunaweza kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga, hivyo kusaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali.


Kuongeza uaminifu na ukaribu wa kihisia: Wakati wa tendo la ndoa, homoni kama oxytocin, inayojulikana kama "homoni ya upendo," hutolewa, ambayo husaidia kujenga uaminifu na ukaribu baina ya wapenzi.


Kuboresha usingizi: Kufanya mapenzi husaidia mwili kupumzika, hivyo kuboresha usingizi kwa sababu ya kupungua kwa msongo wa mawazo na kutolewa kwa homoni za kupumzisha mwili kama prolactin.


Kuboresha afya ya akili: Tendo la ndoa linaweza kusaidia kuboresha hali ya kihisia na kuongeza furaha kutokana na kutolewa kwa homoni za furaha kama serotonin.


Kupunguza maumivu: Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kupunguza maumivu ya mwili kama vile maumivu ya kichwa au maumivu ya hedhi, kutokana na kutolewa kwa homoni za kupunguza maumivu.


Ni muhimu kufahamu kuwa faida hizi hutegemea uwiano mzuri na ushirikiano mzuri katika mahusiano yenye afya na heshima.


Kama unapata shida na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa faida hizi huwezi kuzipata bali utapata hasira na kuweza kulichukia tendo kwa ujumla 


Tutafute kwa namba hizi +255684362870 kwa Ushauri na Matibabu juu ya kurejesha furaha katika ndoa.

Thursday, 8 August 2024

UNAPOAMBIWA UNA HORMONAL IMBALANCE HUWA UNA ELEWA NINI?

 *Unapoambiwa una homoni imbalance huwa una elewa nini?*



Leo ngoja tuangalie suala hili la homoni imbalance. 


Mvurugiko wa homoni kwa wanawake ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa homoni (vichocheo) katika mwili wa mwanamke, hivyo kufanya mabadiliko katika mwili wa mwanamke. 


Tatizo hili kwa kitaalamu hujulikana kama *Hormonal imbalance.*


Mvurugiko wa homoni kwa wanawake huweza kuchangiwa na kutokuwepo kwa usawa katika homoni zifuatazo: 


 *Estrogen, progesterone na testosterone...* 


Ambapo kuzidi au kupungua kwa homoni hizi hupelekea mvurugiko wa homoni (vichocheo) kwa wanawake.


Sababu Zinazopelekea Mvurugiko wa Homoni (Hormonal Imbalance) 


1. Uwepo wa sumu nyingi mwilini 

2. Mtindo mbovu wa maisha

3. Kutofanya mazoezi 

4. Uzito mkubwa

5. Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa

6. Msongo wa mawazo 

7. Utoaji wa mimba

8. Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango 


Dalili za Mvurugiko wa Homoni kwa Wanawake 


1. Kukosa ute wa uzazi

2. Kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa

3. Uke kuwa mkavu sana

4. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

5. Kupata hedhi isiyo na mpangilio mzuri

6. Maumivu makali chini ya kitovu wakati wa hedhi

7. Kukosa hedhi kwa muda mrefu

8. Kupata hedhi yenye mabonge mabonge

9. Kuchagua baadhi ya vyakula

10. Kupata dalili za mtu mjamzito kama maziwa kujaa, kuhisi kichefu chefu, kizungu zungu, n.k

11. Ongezeko la tumbo na nyama uzembe

12. Kupata hedhi wakati wa ujauzito 


Madhara ya Mvurugiko wa Homoni kwa Wanawake 


1. Kutobeba mimba

2. Mimba kuharibika mara kwa mara

3. Kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroids au ovarian cysts) 


Sasa suluhisho lake ni nini?


Kuna suluhisho mbili...

1. Ujisaidie wewe mwenyewe kumaliza hilo tatizo.

 au

2. Sisi tukusaidie kumaliza tatizo hilo.


Chaguo namba moja ni nzuri lakini matokeo yake huwa yanachukua muda sana hadi kuyaona.


Kama hili ndio chaguo lako safi sana, unachohitaji kufanya ni kuhakikisha kila siku unakula ndizi 3 mbivu,


Cabbage (kabichi) bakuli moja (isiyopikwa) na maziwa fresh kikombe kimoja cha chai.


Utatumia ndani ya siku 21 hadi 30 utakuwa sawa kabisa.


Lakini kama unataka matokeo ya haraka na upo tayari sisi tukusaidie basi chaguo la 2 ni bora kwako.


Hapa sisi tutakusaidia kwa kukupatia program ya lishe na tiba.


Ambapo ndani yake unapewa dawa ya kutumia pamoja na lishe ya chakula.


Kwa kawaida program hii bei yake huwa ni Tsh 250,000/=


Lakini kwasababu huu ni mwezi wa 8/8 nitakusaidia kwa Tsh 2000,000/= tu badala ya Tsh 250,000/=


Watu watatu wa mwanzo kulipia nitawapatia dawa ya kuweka homoni sawa na kuondoa infections kwenye kizazi.


Dawa hiyo huwa inauzwa Tsh 290,000/= lakini ukiwa miongoni mwa watu wa mwanzo utaipata bure na utatumiwa bure hadi huko uliko


Kama utapenda kupata ofa hii basi hakikisha unafanya malipo kabla ya tarehe 11/08/2024 saa 6:00 usiku.


Malipo yafanyike kupitia...


M-Pesa No: 0685362860

Jina: Mzamilu Baraka. 


Ukishafanya malipo nitumie majina yako mawili, namba ya simu na mahali ulipo kupitia WhatsApp ili nikutumie mzigo wako.


Mimi mwenye kujali furaha yako, 

.Dr.Mzamilu Baraka